INFORMATION CENTRE
Privatization Commission Service Charter -Kiswahili Version (Mkataba wa Huduma)
MASAA RASMI YA KAZI
Masaa tetu rasmi ya kazi ni kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni siku za kazi huku kukiwa
na na lisali limoja la mapumziko kati ya saa saba na saa nance mchana. Masaa ya kutembelea
- Asubuhi 2.00 asubuhi – 7.00 mchana
- Alasiri 8.00 alasiri – 11.00 jioni
ANWANI YETU NA MAELEZO MENGINE YA MAWASILIANO
Tume ya Ubinafsishaji S.LP. 34542-00100 NAIROBI.
Simu +254 20 2212346/7/8
Kipepesi +254 20 2212237
Tovuti: www.pc.go.ke
Barua pepe:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
LENGO LA MKATABA
Mkataba wa Huduma unalenga kuimarisha kushiriki kwa wadau katika usimamizi bora wa mpango wa
ubinafsishaji hapa Kenya. Hii inawezekana wakati wadau wanafahamu jukumu la Tume kwao na wajibu wanaofaa kutekeleza. Mkataba unaeleza viwango ambavyo wateja na wadau wengine wanaweza kutarajia kutoka kwa Tume ya Ubinafsishaji na yanafafanua jinsi ya kupata habari kutoka kwa Tume. Pia inaeleza jinsi wadau wanaweza kuwasilisha malalamishi yao kwa mujibu wa haki zao na kutoa maoni jinsi Tume inaweza kutoa huduma bora.
SEHEMU KUU ZA MKATABA
- Wajibu wa Tume
- Kazi kuu za Tume
- Wateja na wadau wengine
- Wajibu kwa wateja na wadau wengine
- Jinsi ya kutafuta marekebisho
- Usimamizi na Utathmini
WAJIBU WA TUME
Tume ya Ubinafsishaji imeundwa kama shirika chini ya Sheria ya Ubinafsishaji, 2005. Jukumu la Tume ni kuunda, kusimamia na kutekeleza Mpango wa Ubinafsishaji wa Kenya. Mpango huo unajumuisha orodha ya uwekezaji na mali zilizoidhinishwa kubinafsishwa chini ya Sheria ya Ubinafsishaji.
KAZI KUU ZA TUME Shughuli kuu za Tume ni kama zifuatavyo:
- Unda, simamia na tekeleza mpango wa Ubinafsishaji;
- Tayarisha na tekeleza mapendekezo mahususi ya Ubinafsishaji kulingana na mpango wa Ubinafsishaji;
- Tekeleza majukumu mengine kama yalivyoelezwa na Sheria; na
- Tekeleza majukumu mengine ambayo Tume inadhania yanafaa ili kuendeleza Mpango wa Ubinafsishaji.
Ili kutekeleza majukumu haya, Tume ina Wanachama wa Tume ambao hutoa mwongozo mwafaka kwa wafanyikazi kutekeleza wajibu huu.
KANUNI ZA MKATABA
- Uadilifu: tutakuwa watu waadilifu.
- Uwazi: maamuzi na vitendo vyetu vitafanywa kwa uwazi.
- Uwajibikaji: tutawajibikia maamuzi na vitendo vyetu.
- Utaalamu: tatika vitendo na kuhusiana kwetu kwote, tutaimarisha adabu ya utaalamu.
- Usawa: tutaonyesha uthabiti na usawa katika shughuli zetu zote.
TAARIFA YA NIA
Tutajizatiti kuweka mazingira ya kufaa kwa wafanyikazi wote kwa kuwapa mbinu bora za utendakazi na kuwatia motisha wafanyikazi ili waweze kutoa huduma za hali ya juu kwa wateja wetu.
KUFANYA KAZI NA WANAOTUTOLEA HUDUMA
Tutafanya kazi na wadau wote kuhakikisha tunatoa huduma mwafaka, zenye mpangilio na zinazolingana
tunaposimamia Mpango wa Ubinafsishaji wa nchi.
KUKATAA KABISA UFISADI
Katika kuonyesha uadilifu wetu, tunaahidi kufanya mazingira yetu ya kazi bila ufisadi kwa kufuata amri na masharti yaliyowekwa, sheria na maadili ya utaalamu wakati wote.
KANUNI ZETU
Kulingana na jukumu la Tume, wateja wetu wote wanaweza kutarajia uongozi bora, uwazi, uwajibikaji na usimamizi mwafaka wa Mpango wa Ubinafsishaji. Wadau wetu wakuu na wajibu wetu kwao ni: Taasisi za umma zilizotambuliwa kubinafsishwa
- Muda wa kutosha kufanya mashauriano na kuwasilisha habari na maelezo yanayohitajika
- Kuidhinisha maombi yote kwa wakati unaofaa Kujibu maswali yote kwa wakati unaofaa
- Mashauriano kuhakikisha ujumulishi na umiliki wa shughuli ya ubinafsishaji. Wizara husika ya taasisi zilizotambuliwa kwa kubinafsishwa
- Muda wa kutosha wa mashauriano na kuwasilishwa kwa habari na maelezo yanayohitajika
- Kuidhinisha maombi yote kwa wakati unaofaa
- Kujibu maswali yote kwa wakati unaofaa
- Mashauriano kuhakikisha ujumulishi na umiliki wa shughuli ya ubinafsishaji. Umma unaowekeza
- Usawa na uwazi
- Thamani ya pesa
- Kujibu maswali yote kwa wakati unaofaaWarekebishaji wa soko
- Mashauriano ya kutosha
- Kuwasilisha maombi ya kuidhinishwa kwa wakati unaofaa
- Kujibu maswali yote kwa wakati unaofaa
- Kushiriki habari za sokoUmma wa Kenya
- Thamani ya pesa
- Uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza mpango huo Wafanyikazi
- Haki na usawa
- Mazingira ya kufanya kazi yaliyoimarishwa
- Mfumo wa haki wa kutuza na kuadhibu kulingana na utendakazi
- Kuendelea kuimarisha uwezo
- Mazingira yanayokuza utaalamu na mawazo huruOfisi ya Kitaifa ya Ukaguzi wa Hesabu ya Kenya
- Kutekeleza kikamilifu kanuni za kifedha
- Kujibu maswali yanayohusiana na ukaguzi katika siku saba (7) za kaziWizara ya Fedha
- Kutayarisha na kuwasilisha Mpango wa Ubinafsishaji kwa wakati unaofaa
- Kutayarisha na kuwasilisha maelezo kwa undani ya mapendekezo ya Ubinafsishaji
- Kutayarisha bajeti, mikataba ya utendakazi na ripoti husika kwa wakati unaofaa
- Kutuma maombi ya hati za kisheria na zingine zilizoidhinishwa na ripoti kwa wakati unaofaa
- Kufuata kikamilifu kanuni za kifedha
- Thamani ya pesa
- Muda wa kutosha kufanya mashauriano na kuwasilisha habari na maelezo yanayohi Kujibu maswali yote kwa wakati unaofaa Wauzaji
- Uwazi na usawa
- Malipo yote kufanywa katika kipindi kilichowekwa kwenye mkataba
- Kuwasiliana katika siku saba (7) za kutolewa zabuni
MAJUKUMU YETU
Tumetambua majukumu yafuatayo ili kutuwezesha kuwahudumia vyema wateja wetu:
- Kuwazingatia ipasavyo na kuwaheshimu wateja inavyostahili na kuwapa hadhi zao za kibinafsi
- Kuwa waaminifu na wenye kusaidia
- Kutimiza utaalamu katika kazi yetu
- Kuwa wa vitendo na kujali mahitaji ya wateja wetu
- Kujibu barua katika siku saba (7) za kuipokea
- Kushughulikia mara moja mikutano na kuomba radhi ikiwa itaahirishwa ama itachelewa
- Kuwashughulikia wateja wote kwa usawa na
- kuwa waangalifu hususan kwa walio na mahitaji spesheli ama ulemavu wa kimaumbile
- Kukataa kabisa ufisadi kwa kukosa kutarajia, kubali ama kutoa hongo ili kupata huduma
MAJUKUMU YA WATEJA WETU
Tunatarajia wateja wetu kutekeleza majukumu yafuatayo kwetu:-
- Kuonyesha adabu na heshima kwa wafanyikazi wetu
- Kuwa wakarimu na wapole kwa wateja wengine
- Kuwasilisha habari kamili na sahihi kutuwezesha kutenda ipasavyo na kutoa habari zaidi wanapotakiwa kufanya hivyo kwa wakati unaopaswa
- Kuhudhuria mikutano bila kuchelewa wanapoalikwa
- Kufuata sheria, kanuni na masharti
- Kukosa kutoa hongo kwa njia ya zawadi na mapendeleo kwa wafanyikazi ama kutaka hongo ili kupata huduma
- Kutoa habari kuhusu ubora wa huduma
MAJUKUMU YA PAMOJA
Ili kufurahia uhusiano wa kutosheleza na wateja wetu, tutarajia heshima, uangalifu na uvumilivu itadumishwa baina ya pande zote.Wafanyikazi kila mara watavaa vitambulisho vyao vya kazi ili watambulike kwa wazi. Vile vile wageni watatarajiwa kuonyesha tepe za wageni zitakazopeanwa katika sehemu ya mapokezi ya wageni.
HABARI ZA WATEJA/KUSHUGHULIKIA MALALAMISHI
Tunaamini kwamba kuna nafasi ya kufanya marekebisho. Hivyo basi tunakaribisha maoni na mapendekezo kuhusu huduma zetu. Tunahimiza wanaotutumia habari hizi kujitambulisha. Tunakuhakikishia usiri kamili katika kushughulikia habari kama hizi zikiwemo majina na maelezo binafsi. Maoni na mapendekezo yatumwe kwa: Mkurugenzi Mkuu/Afisa Mkuu Mtendaji
Tume ya Ubinafsishaji
S.L.P 34542-00100 NAIROBI
Simu: 254 20 2212346/7/8
Kipepesi: 254 20 2212237
Tovuti: www.pc.go.ke
Barua pepe:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Kutuwezesha kushughulikia habari hizi;
- Tutatoa huduma mwafaka za uhusiano mwema na wateja katika eneo la mapokezi
- Tutatumia kijisanduku cha maoni
Malalamishi yaelekezwe kwa:
Simu: +254 700 315311 +254 731 758970
Barua Pepe:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Malalamishi pia yanaweza kuelekezwa kwa Tume ya Kuchunguza Haki za Kibinadamu katika Orofa la Pili, West End Towers, Waiyaki Way, Nairobi.
Simu: +254 20 2270000/2303000/2603765/24411211
Kipepesi: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.ombudsman.go.ke
S.L.P 20414 - 00200
NAIROBI
UCHAMBUZI WA MKATABA
Mkataba huu unaweza kuchambuliwa. Mwanzoni hili litafanyika kila mwaka kwa usaidizi wa maoni na habari za wateja pamoja na utafiti huru na mashauriano na wateja. Kwa hivyo tunawahimiza wateja na wadau wetu wakiwemo wafanyikazi kutumia mbinu iliyopendekezwa kushiriki majadiliano yenye manufaa na Tume kuhusu viwango tunavyolenga kutimiza, na jinsi wateja wanaweza kuchangia kuviweka ili kutumia mfumo wa utoaji huduma na kuwapa Wakenya Mpango mwafaka wa Ubinafsishaji.
Tume ya Ubinafsishaji
S.L.P 34542-00100, Nairobi.
Jumba la Extelcoms, Orofa ya 11, Barabara ya Haile Selasie
Simu: +254 20 2212346/7/8 Kipepesi: +254 20 2212237
Barua pepe:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.pc.go.ke
Download Privatization Commission Service Charter -Kiswahili Version (Mkataba wa Huduma)